Latest Games :

HEALTH

| 0 maoni

TO VIEW CLICK LINK BELOW

MAHAZIMISHOYA KIFUA KIKUU KANDA YA KUSINI YA FANIKIWA

Dkt. Mponda alisema katika kutekeleza hilo wizara yake inafanya uchunguzi, kutoa dawa ya kuzuia kifua kikuu kwa watu wanaoishi na VVU pamoja na dawa za mseto za kutibu  kifua kikuu hivyo kupunguza muda wa matibabu kutoka miezi nane hadi sita .
Alisema asilimia 88 ya wagonjwa wote wa kifua kikuu wanapona  baada ya kupata matibabu sahii kwa kutumia dawa mseto,kiwango hicho ni zaidi ya lengo la Shirika la Afya Duniani ambalo linataka kila mwanachama kuponyesha angalau asilimia 85 ya wagonjwa wa kifua kikuu, “hivyo sehemu kubwa wagonjwa wa kifua kikuu wanao uhakika wa kupona baada ya kuanza matibabu hata kama pia wana maambukizi ya VVU.
Hata hivyo alisema Wizara imeanza  kununua na kusambaza aina mpya ya darubini za Light Emitting Diode(LED) zenye uwezo mkubwa zaidi wa kugundua vimelea vya kifua kikuu katika makohozi, hadi kufikia mwisho wa mwaka jana asilimia 80 ya hospitali zote za wilaya zilipata darubini hizo mpya na ifikapo mwishoni mwa mwaka huu, hospitali zote zikiwemo za mashirika ya kidini zitapatiwa lengo ni kuzipa hospitali zote nchini uwezo mkubwa wa kuchunguza vimelea vya kifua kikuu.





Tamko la DKT hadji hassan mponda katika siku ya kifua kikuu duniani

TAARIFA KUHUSU CHANJO YA UKIMWI

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuhusu utafiti wa chanjo na tiba ya UKIMWI na kuonyesha kwamba sasa chanjo na tiba imepatikana, ufafanuzi zaidi ni kama ifuatavyo:
  1. Utafiti Kuhusu (HPTN 052)
Utafiti huu uliendeshwa na Taasisi ya Mzio na magonjwa ya kuambukiza ya Marekeani na kushirikisha maeneo ya nchi mbalimbali duniani kutoka Bara la Afrika, Marekani na Asia.
Utafiti ulitokana na ukweli kuwa matumizi ya Dawa za kupunguza makali ya UKIMWI (ARV) hupunguza kuzaliana na kuongezeka kwa virusi vya UKIMWI katika mwili wa binadamu,  hivyo kupunguza maambukizo ya virusi hivyo.  Matokeo ya utafiti huo yameonesha kupungua kwa uwezo wa kumwambukiza mwenzi wako kwa asilimia 96.  Pamoja na habari njema za utafiti ni muhimu jamii ielewe kwamba utafiti huu ulilenga kupata ufahamu zaidi wa kuhusu uwezo wa ARV kupunguza maambukizo.  Hivyo basi, ARV sio chanjo ya UKIMWI.
  1. Kuhusu Chanjo ya UKIMWI
Chanjo iliyotajwa katika baadhi ya Magazeti ni majaribio ya kimaabara yanayohusu wanyama (Jamii ya Nyani) kabla ya matumizi kwa binadamu majaribio haya pia yalifanywa na Taasisi ya Mzio na Magonjwa ya kuambukiza ya Marekani, Programu ya Utafiti wa UKIMWI ya Jeshi la Marekani.  Matokeo ya majaribio hayo yalionyesha kuwa, Kima waliopata chanjo hiyo walikingwa dhidi ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI.
Pamoja na matokeo hayo mazuri ya kutoa mwanga wa kuendeleza tafiti zaidi ni vyema jamii, ikaelewa kwamba majaribio kama haya hayajafanyika kwa binadamu.
  1. Tafiti za chanjo ya UKIMWI Tanzania (Ta MoVac-01 Study)
Majaribio yanafanywa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa magonjwa ya Binadamu ikishirikiana na Chuo Kikuuu cha Tiba cha Muhimbili yanalenga kuainisha usalama na uwezo wa kujenga kinga ya binadamu dhidi ya virusi vya UKIMWI.  Majaribio ya awali yalifanywa nchini Sweden kabla ya kuanza hapa nchini.  Lengo kuu ni kuendeleza tathmini ya usalama na ubora wa chanjo hiyo ya majaribio.  Mtu wa mwisho kuchanjwa ilikuwa ni Januari, 2012, hivyo mchakato wa kuainisha matokeo bado unaendelea.
Hata hivyo jamii inapaswa kuelewa kwamba majaribio yanayoendelea nchini yapo katika hatua za awali hivyo basi, tathmini ya uwezo wa kutoa kinga dhidi ya Virusi vya UKIMWI haijafanyika hadi sasa.
  1. HITIMISHO
Wizara inasisitiza kwamba hadi leo hakuna chanjo wala dawa ya kutibu UKIMWI iliyothibitishwa kitaalamu kuwa na uwezo wa kutoa kinga au kutibu.  Ni vyema jamii ikaendelea kutumia njia/mikakati ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kama wataalam wa Afya wanavyoshauri.

UJIO WA MADAKTALI KUTOKA INDIA

Katibu Mkuu wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Blandina  Nyoni (Katikati) akiongea na Madaktari Bingwa kutoka India baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Mwl. Nyerere, kulia kwake ni Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Deo Mtasiwa, Kushoto ni Mkuu wa Msafara huo Bw. Radhey Mohan.
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imepokea ugeni wa madaktari bingwa 20 wa Moyo, Figo, Mifupa, Saratani, Mishipa ya Fahamu na Upasuaji wa Watoto kutoka India.
Madaktari hawa watatibu wagonjwa waliowahi na wanaosubiria kupelekwa India na Wizara katika hospitali ya Taifa Muhimbili, Taasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI) na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road. Huduma zinaanza kutolewa Jumatatu ya tarehe 31/10/2011 hadi 5/11/2011 saa 3.00 asubuhi  hadi saa 11.00 jioni bila malip



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
Support : Creating Website | chrisantus and friends | Mas Template
Copyright © 2015. Tanzania yetu - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger