MILIPUKO YAENDELEA UKO NIGERIA
Mabomu mawili ya kutegwa garini katika mji wa kaskazini wa Kaduna nchini Nigeria yamesababisha vifo vya watu kadhaa na kujeruhi wengine wengi, maafisa wamesema.
Shirika la Msalaba Mwekundu la Nigeria limesema watu sita wamekufa. Awali huduma za dharura zilisema watu 18 wameukufa.
Milipuko hiyo ambayo imesababisha uharibifu mkubwa, imetokea karibu na eneo lenye hoteli nyingi na kanisa moja.
Eneo hilo limekuwa likishuhudia mizozo ya kidini katika miaka ya hivi karibuni na kusababisha mamia ya vifo vya watu.
Kulikuwa na onyo lililotolewa kuhusu mashambulio hayo katika kipindi cha Pasaka.
Wengi wa waliokufa wanadhaniwa kuwa ni madereva wa pikipiki na kukodisha na omba omba wa mitaani.
Watu walioshuhudia wamesema vitu mbalimbali vilirushwa umbali mrefu kutoka katika eneo la tukio.
Hakuna yeyote aliyejitokeza kudai kuhuska na shambulio hilo, lakini mwandishi wa BBC nchini Nigeria Mark Lobel anasema kundi la wenye itikadi kali la Boko Haram lilisema kuwa lingefanya mashambulio katika kipindi cha Pasaka.
Makundi ya Wakristo nchini humo yamesema yanadhani walipuaji walikuwa wakilenga kanisa moja lililo karibu na tukio, lakini kutokana na hali ya ulinzi iliyopo wakaamua kulipua nje kidogo.
CHANZO BBC SWAHILI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni