Latest Games :
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo SIASA. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo SIASA. Onyesha machapisho yote

ACT WIKI YA UZALENDO TABORA

Jumatano, 15 Aprili 2015 | 0 maoni

ACT imeandaa wiki ya uzalendo ambayo itafanyika mkoa wa tabora
itafanyika tarehe 16/4/2015
wazungumzaji  zitto kabwe
anna mghwira - mwenyekiti
samsom mwigamba - katibu
afande sele pia atakuwepo katika mkutano huo pia na viongozi mbalimbali...

Continue Reading

UDOM SERIKALI YA WANZAFUNZI YAKANUSHA KUHUSU LOWASSA

Ijumaa, 10 Aprili 2015 | 0 maoni


VYUO VIKUU DODOMA KULAANI KUHUSISHWA KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU VYA DODOMA NA KUMUOMBA MH.  LOWASA KUGOMBEA URAIS.



Ndugu Waandishi wa habari, Tunapenda kutanguliza shukrani za dhati kwenu kwa kufika katika eneo hili kutusikiliza.Mbele yenu ni viongozi wa serikali za wanafunzi kutoka Vyuo vikuu mbalimbali vilivyopo mkoani                               Dodoma.Ndugu waandishi wa habari,si kawaida na wala mazoea kwa marais na viongozi wa serikali za wanafunzi kutoka vyuo tofauti kukutana kwa pamoja na kuzungumza na nyie wanahabari kama inavyotokea hii leo.
Ndugu wanahabari,siku ya Jumapili ya tarehe 22 mwezi huu wa 3,kundi la watu waliojitambulisha kama ni wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma walijikusanya nyumbani kwa mh;                 Lowasa na kutoa matamko mbalimbali ikiwa pamoja na kuutangazia uma wa watanzania kuwa sisi wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma tunamuunga mkono na tunahitaji Lowasa awe rais wetu sambamba kumchangia pesa.
Ndugu wanahabari,Tunapenda kukanusha kuwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma kwa ujumla wetu hatukuhusika na jambo lile na kama viongozi wa serikali za wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya mkoa huu wa Dodoma,Tunapinga na kulaani kitendo cha watu wachache kwenda kutuingiza sisi             wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma katika jambo ambalo halituhusu na wala si lililotuleta hapa Dodoma.Sisi kama wasomi ambao jamii inatutegemea kama kioo hatuwezi kuandamana na kujikusanya kwenye nyumba ya kiongozi na kumuomba agambee urais, wakati tunajua fika sisi hatuhusiki na uteuzi wa wagombea ndani ya taasisi yao.Kilichofanyika ni kuudanganya uma wa watanzania na taasiasi yake kupitia kivuli cha vijana wachache kutoka vyuo vya hapa                          Dodoma,waliolipwa pesa ili waweze kuwa kava la tukio lile.
Ndugu wanahabari,Mkoa wa Dodoma unavyuo vikuu visivyopungua 8,Na jumla ya wanafunzi wote tunaosoma katika vyuo vya Dodoma ni zaidi ya wanafunzi  35,000.Chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) pekee yake kinawanafunzi wasiopungua 22,000.Idadi ya watu waliojikusanya nyumbani kwa Mh: Lowasa siku ya tarehe 22-03-2015 haizidi watu 230 wakiwemo Wamachinga na Wenyeviti wa Jumuiya za wazazi, kama vyombo vya habari vilivyoripoti. Ukiwatoa Wamachinga na Wenyeviti wa Jumuiya za wazazi waliotoka mikoa mbalimbali,idadi ya wanafunzi waliokuwepo kwenye tukio lile hawazidi 150.Idadi hii ni sawa na asilimia 0.4 ya wanafunzi wote wanaosoma vyuo vikuu vya Dodoma.Ndugu wanahabari,kwa akili ya kawaida kabisa asilimia 0.4 ya wanafunzi wa vyuo vikuu ndio waliokuwa pale.Tunashangazwa na dhambi tusiyoitenda tunayobebeshwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma ambao kwa sasa tupo bize na msimu mpya ya masomo wenye changamoto mbalimbali.
           Ndugu wanahabari,sisi kama vijana wasomi na watu tunaotegemewa na jamii zetu tutakusanyika katika kujadili na kuchambua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii yetu na sio kukusanyika kwa ajili ya mwanasiasa ambaye sifa zake na uhadilifu wake unatiliwa shaka katika jamii.
          Tunaomba mlijulishe Taifa, kuwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma hatujahusika na tukio lile isipokuwa wanafunzi wachache walitumika kwa kupewa pesa na wahusika wa tukio lile.Tunataka Taifa lijue hatupo tayari kutumia elimu zetu kulitia upofu taifa letu.Waambieni mama zetu na baba zetu huku vijijini kwetu kuwa tumekuja kutafuta elimu ili ituwezeshe kuwakomboa wao na sio kutumika na               Wanasiasa kwa malengo yao.Tunatambua haki ya mwanafunzi kuamua na kufanya shughuli za kisiasa nje ya maeneo ya vyuo, lakini hatukubaliani na wanafunzi wachache kuchafua na kuwapaka matope maelfu ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya Dodoma ambao hawajahusika na tukio lile.Hii sio haki na haikubaliki.
       Vilevile tungependa kutumia fursa hii kuwaasa wanafunzi wenzetu popote pale nchini, makundi mbalimbali ya kijamii (wakulima, wafugaji, wavuvi, wamachinga, wasanii, n.k), zikiwemo taasisi za dini kwamba watu wachache kuzungumza kwa niaba ya makundi juu ya mambo yanayogusa maamuzi ya mtu binafsi.
Mwisho tunatoa wito kwa wanafunzi wenzetu wote kujitambua na kutumie muda wetu kwa mambo ya msingi na muhimu kwa ustawi wa Nchi yetu. Na kuonesha jinsi wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Dodoma walivyokasilishwa na jambo hili, Tamko hili limesainiwa na wanafunzi 7821 toka vyuo mbali mbali vya Dodoma.Majina ya sahihi za wanafunzi zimeambatanishwa. Tusikubali kutumika na wanasiasa wa aina hii..
Asanteni
Mungu ibariki Tanzania,Mungu vibariki vyuo vikuu vya Dodoma.
Kwa niaba ya wawakilishi wa serikali za Wanafunzi Chuo cha Mipango,Chuo cha Madini, Chuo cha Hombolo,Chuo kikuu cha Dodoma(UDOM) na CBE.

DANIEL DANIEL   -Rais wa Saint Jonh’s University
26/03/2015
Continue Reading

Barua ya serikali ya wanafunzi IFM kukanusha kumuunga mkono LOWASA.

| 0 maoni

Barua ya serikali ya wanafunzi IFM kukanusha kumuunga mkono LOWASA.


Continue Reading

MKUTANO WA CHADEMA ARUSHA

Jumamosi, 7 Aprili 2012 | 0 maoni

MKUTANO ULIOFANYIKA ARUSHA

wamesema kuwa kuna wanachama ccm walioamia
kwenye chama chadema Wasema wameama ccm kwa kumkataa ROWASA
siosiri mati ulikuwa mkubwa sana uko arusha na mkutano umeshaisha ambao
ulikuwa unarushwa kupitia ARUSHA MAMBO FM ONLINE
lakini kuna muda ilisumbua kidogo sikuweza kupata taarifa ya mkutano zaidi kutokana
na matatizo ya urushaji wa matangazo kwa kutumia internet ulisumbua katika
radio ya RUSHA MAMBO FM



lakini wanachama wanaotaka kuamia chadema wameambiwa wafuate kadi za kujiunga
wameambiwa waende ofice ya chama GALNALO
mheshimiwa nassari mbunge wa chadema  juumanne ataelekea bungeni kuapishwa bungeni
chadema wametangaza kuwa wana arusha watakao taka kuwasindikiza mbunge wa arumeru msafala utanzia
majani ya chai saa mbili kamili asubuhi kuelekea dodoma
Continue Reading

WANAOTAKA UBUNGE AFRIKA MASHALIKI KUPITIA CHADEMA

Alhamisi, 5 Aprili 2012 | 0 maoni


TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MWISHO WA UREJESHAJI FOMU ZA WAGOMBEA WA UCHAGUZI WA WAJUMBE TISA (9) WATAKAOIWAKILISHA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI (EALA) KUPITIA CHADEMA  


Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinawatangazia wanachama wote waliochukua fomu za kugombea ujumbe wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) kupitia CHADEMA kwamba muda na siku ya mwisho ya kurejesha fomu za uchaguzi husika ngazi ya taifa ni tarehe 6 Aprili 2012 siku ya juamamosi saa 10:00 Jioni.

Uchukuaji na urejeshaji wa fomu za uchaguzi husika unaendelea kupitia ofisi za mikoa na makao makuu ya CHADEMA baada ya fomu za kuomba nafasi ya ubunge wa Afrika Mashariki kusambazwa katika ngazi husika. Mwanachama yoyote atakuwa na sifa za kustahili kugombea na kuchaguliwa kuwa mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki endapo anazo sifa za kustahili kuchaguliwa kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 67 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; si Waziri katika serikali; si mtumishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na ana uzoefu uliothibitishwa au moyo wa kupenda kuimarisha na kuendeleza malengo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. 

Mkutano wa chama utakaoidhinisha uteuzi wa mwisho wa wagombea kwa mujibu wa masharti ya katiba na kanuni za chama utafanyika tarehe 9 Aprili 2012. Izingatiwe kuwa tarehe 12 Machi 2012 Katibu wa Bunge alitoa Taarifa kwa Umma kwamba, Uchaguzi wa wajumbe tisa (9) watakaoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki utafanywa na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, wakati wa Mkutano wake wa Saba utakaofanyika Dodoma, kuanzia tarehe 10 hadi 20 Aprili, 2012. 

Kwa mujibu wa kanuni za utaratibu wa uteuzi wa wagombea wa uchaguzi wa nafasi za ubunge katika Bunge la Afrika Mashariki, chama chochote chenye haki ya kusimamisha wagombea kinaweza kuwasilisha wagombea watatu kwa kila nafasi wazi katika makundi yafuatayo: 
  • Kundi A-Wagombea Wanawake
  • Kundi B-Wagombea wa Zanzibar
  • Kundi C-Wagombea wa Vyama vya Upinzani
  • Kundi D-Wagombea wa Tanzania Bara
Uchaguzi huo wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki unafanyika kwa kuzingatia kuwa maisha ya Bunge hilo lililoingia madarakani mwaka 2006 yatafikia ukomo wake 04 Juni, 2012. 

Taarifa imetolewa kwa vyombo vya habari na: 

John Mnyika 
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi 

03/04/2012 



Continue Reading

HONGERA BWANA JOSHUA NASSARI

Jumatatu, 2 Aprili 2012 | 0 maoni


Baada ya masaa na wasiwasi mwingi hatimaye Mkurugenzi wa Uchaguzi amemtangaza Bw. Joshua Nassari (CHADEMA) kuwa Mbunge mteule baada ya kumshinda Siyoi Sumari wa CCM. Bw. Nassari alitoa mojawapo ya hotuba za kusisimua kutolewa baada ya ushindi. "Tulianza na Mungu, Tutamaliza na Mungu" amesema Mbunge huyo ambaye ni miongoni mwa wabunge vijana zaidi nchini.


Continue Reading

SIASA IMEKUWA SEHEMU YA KUPEANA MATUSI

| 2maoni


Mh. Livingstone Lusinde akimwaga Sera za CCM Arumeru


siasa imekuwa sehemu ya kupeana maneno ya kiuni na hili linaonyesha zaili kuwa viongozi wetu maarifa hawana  mbunge mwenye akili timamu hawezi akapanda jukwaani na kuongea maneno machafu kama haya

Continue Reading
 
Support : Creating Website | chrisantus and friends | Mas Template
Copyright © 2015. Tanzania yetu - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger