Latest Games :
Home » » BODI YA WAKURUGENZI TANZANIA TOURIST BOARD YAZINDULIWA

BODI YA WAKURUGENZI TANZANIA TOURIST BOARD YAZINDULIWA

Ijumaa, 6 Aprili 2012 | 0 maoni

TANZANIA TOURIST BOARD


Baada ya kutangazwa kwa Bodi mpya ya wakurugenzi ya Bodi ya Utalii hivi karibuni, Bodi hiyo imezinduliwa rasmi leo tarehe 5 Aprili 2012 na Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Ezekiel Maige (Mbunge). Uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi mkuu wa wizara hiyo uliopo makao makuu ya Wizara (Jengo Mpingo)
Mh. E. Maige Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii akitoa hotuba yake wakati akizindua Bodi Mppya ya Wakurugenzi ya Bodi ya Utalii Tanzania.




Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi,  Bodi ya Utalii Tanzania Balozi Charles Sanga akihutubia mara
baada ya uzinduzi wa bodi hiyo, mwenye tabasamu kulia kwake ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii, Tanzania  Dkt Aloyce K. Nzuki
Picha ya pamoja kati ya Uongozi wa Wizara na Bodi mpya iliyozinduliwa (Mstari wa mbele wa tatu kulia ni Mh. E. Maige Waziri wa Maliasili na Utalii (Mbunge), kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. M. Tarishi na Kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Nuru Millao wengine ni Mwenyekiti mpya wa Bodi ya wakurugenzi Balozi Charkes Sanga, Mkurugenzi wa Idara ya Utalii Bw. Ibrahim Mussa, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Mh. K.S Teleli (Mbunge) na mwisho kulia ni Dkt Aloyce Nzuki- Mkurugenzi Mwendeshaji Bodi Utalii Tanzania.
Mstari wa nyuma kuanzia kulia ni Prof. Isaya Jairo, Bi Teddy H. Mapunda, Mh. Abdulkarim E.H Shah na Bw. Samweli D.J. Diah
 SOURCE TTB


Share this article :

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

 
Support : Creating Website | chrisantus and friends | Mas Template
Copyright © 2015. Tanzania yetu - All Rights Reserved
Template Modify by Creating Website
Proudly powered by Blogger