TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MWISHO WA UREJESHAJI FOMU ZA WAGOMBEA WA UCHAGUZI WA WAJUMBE TISA (9) WATAKAOIWAKILISHA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI (EALA) KUPITIA CHADEMA
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinawatangazia wanachama wote waliochukua fomu za kugombea ujumbe wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) kupitia CHADEMA kwamba muda na siku ya mwisho ya kurejesha fomu za uchaguzi husika ngazi ya taifa ni tarehe 6 Aprili 2012 siku ya juamamosi saa 10:00 Jioni.
Uchukuaji na urejeshaji wa fomu za uchaguzi husika unaendelea kupitia ofisi za mikoa na makao makuu ya CHADEMA baada ya fomu za kuomba nafasi ya ubunge wa Afrika Mashariki kusambazwa katika ngazi husika. Mwanachama yoyote atakuwa na sifa za kustahili kugombea na kuchaguliwa kuwa mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki endapo anazo sifa za kustahili kuchaguliwa kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 67 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; si Waziri katika serikali; si mtumishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na ana uzoefu uliothibitishwa au moyo wa kupenda kuimarisha na kuendeleza malengo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mkutano wa chama utakaoidhinisha uteuzi wa mwisho wa wagombea kwa mujibu wa masharti ya katiba na kanuni za chama utafanyika tarehe 9 Aprili 2012. Izingatiwe kuwa tarehe 12 Machi 2012 Katibu wa Bunge alitoa Taarifa kwa Umma kwamba, Uchaguzi wa wajumbe tisa (9) watakaoiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki utafanywa na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, wakati wa Mkutano wake wa Saba utakaofanyika Dodoma, kuanzia tarehe 10 hadi 20 Aprili, 2012.
Kwa mujibu wa kanuni za utaratibu wa uteuzi wa wagombea wa uchaguzi wa nafasi za ubunge katika Bunge la Afrika Mashariki, chama chochote chenye haki ya kusimamisha wagombea kinaweza kuwasilisha wagombea watatu kwa kila nafasi wazi katika makundi yafuatayo:
Taarifa imetolewa kwa vyombo vya habari na:
John Mnyika
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
03/04/2012

- Kundi A-Wagombea Wanawake
- Kundi B-Wagombea wa Zanzibar
- Kundi C-Wagombea wa Vyama vya Upinzani
- Kundi D-Wagombea wa Tanzania Bara
Taarifa imetolewa kwa vyombo vya habari na:
John Mnyika
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi
03/04/2012
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni